Recent Comments

Muuaji msikitini Mwanza alivyowaponyoka polisi’

Gazeti hilo limeripoti kuwa jeshi la polisi mkoani Mwanza limesema mtuhumiwa wa ujambazi waliyemkamata kwa matukio mbalimbali ya uhalifu yakiwamo ya uporaji maduka ya miamala ya kifedha na mauaji ya watu watatu msikitini, Hamis Juma, ametoroka chini ya ulinzi mkali wa polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Ahmed Msangi alisema juzi mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Nyegezi, alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka walipojificha wenzake katika mlima Kiloleli Nyasaka kata ya Kirumba wilayani Ilemela.
Msangi alisema baada ya polisi na mtuhumiwa huyo wa ujambazi kufika eneo la tukio saa 8:00 usiku ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka ndipo alipopata mwanya wa kutoroka.
Aidha alisema katika mapigano hayo, polisi walikamata bunduki aina ya shortgun iliyokatwa mtutu na kitako na risasi moja kwenye chemba iliyotupwa na majambazi hao.
Share on Google Plus

About BongoVitimbi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment